Jumatatu, 8 Mei 2017

HATIMAYE BAADHI YA MAMBO AMBAYO YALIWEZA KUSABABISHA YAGUNDULIKA

Wakuu,
Kabla ya yote, natoa pole kwa familia, Ndugu na
marafiki waliofikwa na msiba huu katika ajari ya
Bus.
Lakini pia nitoe pongezi kwa watanzania wenzangu
ambao kwa namna moja au nyingine wameshiki
katika kuwatia moyo na kuwapa pole wafiwa.
Ni kweli tujuavyo kwamba ajari haiepukiki lakini
kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia
kuna baadhi ya ajari zinaepukika.
Kwa utafiti mdogo niliyo ufanya nimegundua baadhi
ya mambo ambayo yamepelekea kutokea kwa vifo
vingi vya wanafunzi hawa.
1. SEAT BELT
Kuna kila dalili Bus haikuwa na seat belts, na hata
kama ilikuwepo wanafunzi hawakufunga ile
mikanda. Ukiangalia mwonekano wa Bus, sehemu
kubwa iliyopondeka ni sehemu ya Mbele na karibia
robotatu ya Bus halijapondeka Sana. Sasa kama
kila mwanafunzi angekuwa kafunga mkanda
wanafunzi waliokaa siti za nyuma wengi
wangepona.
Kwa sababu hakukuwa na seat belt ilipelekea
wanafunzi na walimu wao wote kulushwa mbele ya
gari baada ya gari kukita kwenye kolongo.
2.UZEMBE WA DEREVA
Kuna kila dalili palikuwa na uzembe. Dereva alikuwa
speed kubwa na gari likamshinda kwenye kona
ukizingatia na ubichi wa barabara kutokana na
mvua zinazoendelea.
OMBI LANGU:
wazazi/Waalimu tuwe makini muda wote na hawa
watoto wetu hasa kwenye hizi School Bus, kuna ka
tabia ka kulundika watoto, unakuta seat ya watu
wawili watoto wamewekwa wanne. Inapelekea
watoto kushindwa kufunga mikanda.
Mungu atusaidie!

SEHEMU YA KWANZA YA SIMULIZI TAMU INAYOKWENDA KWA JINA LA ASIA DIGITALI


CHOMBEZO: ASIA DIGITALI SEHEMU
YA KWANZA
CHOMBEZO: ASIA DIGITALI
MTUNZI: George Iron Mosenya
SEHEMU YA KWANZA.
Joto lililokuwa katika chumba kikubwa cha ‘internet
café’ liliwafanya wateja wajipepee kwa kutumia
makablasha kadhaa waliyoingia nayo ama kuyakuta
katika chumba kile.Joto lile lilikuwa kero kwa kila mteja
mle ndani, lakini kwa mtu mmoja tu n’do lilikuwa
sherehe.Alikuwa ameyaona mawindo sahihi
kabisa.Mawindo ambayo yangepewa ushirikiano mkubwa
na lile joto.
Mkabala na mahali alipokuwa amekaa alitazamana na
kijana wa makamo ambaye afya na mavazi yake pekee
yaliidhinisha uwezo wa yeye kuwa ameegesha gari nzuri
nje ya jingo lile na mfukoni hakukosa noti kadhaa zenye
uzito wa kuitwa pesa. Jasho lilikuwa likimtiririka na
alikuwa amejikita katika kujipangusa kwa kutumia leso
yake.
Kabla umeme haujakatika kijana huyu alifanya siri na
kuchungulia mapaja meupe ya binti huyu ambaye
hakuteswa na joto lile bali ilikuwa sherehe. Wakati
kijana huyu akidhani kuwa alichofanya kilikuwa siri
sana…jicho kali na la kitapeli la binti yule liliweza
kushuhudia matamanio ya kijana yule.
Sasa umeme ulikuwa umekatika, joto limetawala binti
akaamua kuitumia nafasi.
“Atanijua mimi nd’o Asia.” Alijisemea wakati akifungua
baadhi ya vishikizo vya blauzi yake. Alifanya hivi huku
akkizuga kuwa anateswa sana na lile joto.Maziwa yake
ambayo pia yalikuwa meupe pee yalionyesha mchirizi
ambao asilimia kubwa ya wanaume wakiutazama
hutamani kuona na kinachoendelea chini.
Asia hakuachia uhondo wote, alimuacha yule kijana
katika mtihani wa matamanio.Kwa jicho lililofuzu
kulaghai wanaume aliweza kuiona suruali ya kitambaa ya
yule kijana ikitoka katika kutepeta na
kukakamaa.Akafanya tabasamu la kusanifu, akijifanya
anaitazama simu yake.Kijana wa watu hakujua kama
anachezewa akili.“Kashajileta pumbavu zake.”
Aliendelea kufanya tathmini.
Mara akaitupa karata ya mauaji ambayo aliamini kwa
namna yoyote lazima yule mwanaume atajiingiza katika
himaya yake.Asia kwa kutumia vidole vyake vyenye
kucha bandia alibofya simu yake iliyokuwa katika
mkoba.Ikaanza kuita akaichomoa.
“Hellow……..mwenzangu….yaani najaribu kucheki Bro
Smith, Skype umeme nao huko umekatika, nimemcheki
kwenye simu, dah network ya Germany sijui vipi. Mbona
yamenishuka mwenzako.” Asia aliongea kwa sauti
nyororo inayobembeleza na bila shaka ilikuwa
inatangaza maisha bora anayoishi kwani alikuwa katika
kudeka.
Kimya kikatanda kama anayesikilizia kitu fulani kutoka
upande wa pili. Kisha akafanya cheko, cheko
lililoyaruhusu maziwa yake kifuani kucheza kidogo,
akafanya kuiegemea simu akayarekebisha. Jicho lake
kama kawaida likamchungulia muhusika wake.
Muhusika alikuwa amesahau kujipepea, alikuwa
anatokwa jasho na alikuwa katika kushangaa.“Mi
nataka kuondoka hapa, maana hakuna jipya, ..”
akaweka kimya tena. Kisha akaendelea.“Naenda Msasani
sahivi, lakini shoga mwenzio si unicheke kabisa
mapema….sina gari hapa najishaua tu….maza kaenda
nalo Mwanza, na mimi kuendesha ka Lexus kake
sitaki.”Akaweka nukta tena.
“Mh…atoke wapi wa kunichukua wewe……naenda zangu
kupanda daladala mie. Nitafanyaje sasa………baadaye
basi Shosti.” Alimaliza maongezi akaufunga mkoba wake
baada ya kuwa ameweka simu ndani yake.
Akasimama, akapiga hatua kadhaa, taratibu huku
akiruhusu nyamanyama zilizovimbiana kwa nyuma na
kumfanya apendeze zikitikisika kwa fujo. Yote haya
yalitokea ili fulani aweze kuona.Macho hayana pazia,
mikono ikamwenda kinywani, akakunja kunja sharubu
zake, kisha mkono mmoja ukamponyoka na kuifikia
suruali yake, akauingiza ndani na kusawazisha
mambo.Macho ya Asia hayakukosea kumsoma, alikuwa
ametamanika.
Kijana akasimama, akajifanya kunung’unika kutokana
na huduma mbovu walizopata, hakukumbuka kudai pesa
zake.Akapiga hatua kubwa akamfikia Asia.“Vipi dada na
wewe wamekuchosha nini? Watu gani hawa yaani umeme
umekatika hawawashi jenereta. Aaaargh.”
Alilalamika.Asia akajichekesha kisha akasonya.“It’s
boring…..yaani dah basi tu….but it sucks….” Akatema
maneno, Kiswahili kwa mbali ung’eng’e mwingi.
Wakaendelea na mada ya kuwalalamikia watoa huduma
hizo. Hadi wakaufikia ukumbi ule wa kuoneshana nani ni
nani.Ilikuwa sehemu ya kuegeshea magari.“Kwani dada
unaelekea wapi.” Kijana ambaye alikuwa
hajajitambulisha jina akauliza.“Msasani, ngoja
nikapate kero nyingine ya kugombania magari. We
unaenda pande zipi au safari yetu moja?” aliuliza Asia
huku akijua nini kinafuata.
“Mimi nafika Namanga hapo. Kuna watu naenda kuonana
nao hivi mara moja. Dah hizi kazi hizi.” Alilalamika
katika namna ya kujifagilia njia.“Poa kumbe gari moja
twende ukanisaidie kuwania siti.”
Jamaa kusikia vile akajikoholesha kisha akamwonyesha
Asia kwa kutumia kidole cha shahada, gari aina ya Noah
nyeupe ikiwa imetulia ikimsubiri mmiliki. “Mwenzangu
heri yako…poa kaka siku nyingine lakini hapa sirudi
tena aisee.” Alisema Asia huku akiondoka.“Twende
nikusindikize kidogo bwana..” alisihi yule kijana.
Asia akajifanya kufikiri kidogo kisha akauliza swali la
kijinga.“Hamna mahali unapita maana mimi nina haraka
kweli.”“Naenda moja kwa moja.”Asia akakubali,
wakaongozana garini.Safari ya kuelekea Msasani.
Ndani ya gari maongezi ya hapa na pale
yaliendelea….Asia kwa kutumia simu yake akafanya
jambo jingine lililompelekea kujikuta anahamishiwa
rasmi katika timu nzima ya digitali.Akaandika ujumbe
baada ya dakika moja simu yake ikaita.
“Mh…sorry..simu yangu inatatizo la speaker I hope
sitakuboa nikitumia loud.” Asia alisema huku akiyafinya
macho yake katika namba ya kumhangaisha mwanaume
dhaifu. “Aaah…hata usijali ongea tu….” Alijibu.Asia
akapokea simu akaiweka katika spika kubwa.“Ehe
nambie….” Akaanzisha maongezi. “Peter kanipigia
mwenzangu…..”“Anataka nini?”
“Asia jamani…msamehe mwenzako …..kabembeleza
sana ujue….” Sauti kutoka upande wa pili ikasihi.”
“Jackline, nakuheshimu sana…nakuomba kwa heshima
ya urafiki wetu…usinambie lolote kuhusu huyo tapeli wa
mapenzi, Jack umekuwa shahidi wa ujinga alionifanyia
Peter….umeshuhudia uchafu wake wote…leo hii
unamwombea msamaha…Jack kweli umenichoka kiasi
hicho, amekulipa huyo Peter umwombee msamaha……ok
Jack labda niseme neno moja tu….ulifurahia
alichonifanyia sivyo…..Mbarikiwe sana “ Akamaliza huku
analia, akaikata simu, uso ukiwa mwekundu, ngozi yake
ya rangi ya chungwa ikikosa ustahimilivu na kuchafuliwa
na machozi…kilikuwa kilio haswa. Asia alikuwa analia.
Kijana aliyekuwa anaendesha gari ambaye mwanzoni
alikuwa amemtamani Asia alijikuta akipagawa, mara
akaiegesha gari pembeni.Vioo vyeusi tii…nani atajua
kinachoendelea ndani. Nd’o uzuri wa tinted Akaanza
kumbembeleza Asia. Akamsihi sana asilie, Asia akawa
analia huku anawalaani wanaume wote. Alimlaani Peter
hadi yule kijana naye akamsaidia katika kumlaani.
“Mpendwe vipi nyie wanaume …mnataka roho zetu…
mnataka tufe nd’o mjue kuwa mlipendwa au? Yaani
mtalaaniwa nasema atalaaniwa huyo Peter, kwa chozi
hili linalonitoka mimi Asia…Peter alitaka nini mimi
nikamnyima, pesa zangu za kutumia chuo, pesa za
kujaza gari mafuta zote nimempa mimi. Alitaka nini
sasa, nimepigwa na dadiii mimi mamii akanichukia, kaka
zangu wamenipiga makofi mimi. Kisa Peter,
Peter….aah…” Asia aliendelea kulaani maneno
yaliyomsulubu yule kijana.
Akiwa hajui cha kufanya Asia akiwa analia alimlalia,
alimlalia kifuani, zile chuchu alizoziona kwa kuibia kule
‘internet café’ sasa zilikuwa zimemlalia zikimchoma
katika namna ya kuleta hamasa, kucha za bandia za Asia
zikalifinyafinya shingo lenye afya la yule kijana.
Pumzi za kupishana ndani na nje zikawa zinatesa katika
sikio la yule kijana. Sasa alianza kupagawa. Huyu Asia
alikuwa anajibembeleza ama.Akawa katika sintofahamu.
Nani atampa jibu?Asia akalisikia paja lake likiguswa na
kitu ambacho hakikuwepo hapo awali. Hakushtuka
Akafanya tabasamu jepesi kisha akamzomea yule
jamaa.Hicho kitu kilivimba kutoka katika suruali
nyepesi.
“Bwege linawahi kweli kupata hamu hili.” Asia alikebehi
kimya kimya.Hamu zikamzidi yule kijana, mara naye
akakumbatia, mara akakumbatia kwa nguvu zaidi. Mara
akaanza kunena katika lugha za maajabu zisizojulikana
kitaifa wala kimataifa.
Mikono yake ilikuwa ikitalii katika mzigo wa titi mbili
ndogo za Asia.Afadhali yeye alikuwa ananena
kilugha.Asia alikuwa hoi kama aliyezirai.Jamaa akajua
kuwa Asia kakolea.Laiti kama angejua kuwa Asia
anatumia mbinu ya kidigitali, basi ni heri angebaki
katika dunia ya analojia aliyokuwa anaishi awali.
“Baby…..Baby…..unaniua
mweenzio….unaniaaa…..pliiz stop…..” “Am sore bebi…
am sore vere sore….me you know…” Jamaa akajaribu
kiingereza asichokijua, Asia akataka kupitiwa na
kicheko.Akajikaza. Alikuwa kazini.
Mkono wa jamaa ukapenya katika mapaja…..Asia
akajua jamaa anataka kumpima kina cha kisima na
kutazama kama kina maji ama ni kikavu.“Bwege asije
akanichafua bure..akavuka mipaka…..”Asia digitali
akacheza kidigitali, alishagundua kuwa jamaa ni
mwepesi sana.
Ulimi mkali kama ule wa kinyonga, ulimi ambao
ulishausema uongo hadi uongo ukauzoea ukazama katika
sikio la yule jamaa.“Uwiiiiiii….ooooohhh yeees..” jamaa
akaganda kama roboti, mkono haukwenda mbele wala
kurudi nyuma.Akazidi kunena kwa lugha zake zisizokuwa
za kiroho.Asia akagundua kuwa amefanikiwa kwa kiasi
kikubwa.Akafanya tekniki ya mwisho.Akajibandua katika
mwili wa jamaa….akaanza kujifuta midomo, na
kujifanya anaona aibu……jamaa kaduwaa tu hajui
digitali inakwenda vipi. Analojia ilikuwa imemwathiri.
Jamaa akawa na aibu za kweli, suruali ilikuwa wima
sana. Akajitazama, shughuli ikaja je airekebishe ama
aicha ilivyo………
****Huyu ndiye Asia Digitali…….je historia yake
inaanzia wapi…ni lini alihamia digitali…chanzo cha
kuaicha analojia ni kipi???
****NI MWANZO TU WA CHOMBEZO HILI LA AINA YAKE
AMBALO LINAKUWEKA KATIKA HALI MBILI, KICHEKO NA
HISIA……..KAZI NI KWAKO…. ENDELEA KUTEMBELEA  www.joh53.blogspot.com

AJALI MBAYA ILIYOTOKEA KARATU MKOANI ARUSHA NA KUUWA WANAFUNZI

AJALI Karatu: Coaster yaua wanafunzi na walimu(karibu wote)
Nimepata habari isiyo na shaka kuwa gari aina ya coaster limeua watoto karibu wote waliokuwa wanaelekea mjini Karatu kwa ziara ya kimasomo, taarifa zinasema wamebaki watoto wawili tu wengine wamefariki, shule inaitwa Lucky Vincent Nursery & Primary School ipo Arusha ni medium schools,kwa wenye updates tunaomba mtupe Picha: Soon ntaziapload ni ajali ya mda huu Mungu awalaze mahali pema peponi ---------------------- UPDATE: Coaster ina jumla ya abiria 58 na wote wanasadikiwa wamefariki,maiti zimepelekwa hospitalini na watu wameondoka eneo la tukio,mvua inanyesha UPDATE: Picha zinakuja soon ripota yuko eneo la tukio.. ......................... UPDATES:Magari ya polisi yametanda kila kona na maiti zimebebwa na magari ya polisi Tayari kuhifadhiwa ................... UPDATES:Ni watoto wanne(4) wanasadikiwa wako hai ila wako mahututi kabisa na kuna wasi wasi vifo vikaongezeka
https://www.joh53.blogspot.com