Wakuu,
Kabla ya yote, natoa pole kwa familia, Ndugu na
marafiki waliofikwa na msiba huu katika ajari ya
Bus.
Lakini pia nitoe pongezi kwa watanzania wenzangu
ambao kwa namna moja au nyingine wameshiki
katika kuwatia moyo na kuwapa pole wafiwa.
Ni kweli tujuavyo kwamba ajari haiepukiki lakini
kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia
kuna baadhi ya ajari zinaepukika.
Kwa utafiti mdogo niliyo ufanya nimegundua baadhi
ya mambo ambayo yamepelekea kutokea kwa vifo
vingi vya wanafunzi hawa.
1. SEAT BELT
Kuna kila dalili Bus haikuwa na seat belts, na hata
kama ilikuwepo wanafunzi hawakufunga ile
mikanda. Ukiangalia mwonekano wa Bus, sehemu
kubwa iliyopondeka ni sehemu ya Mbele na karibia
robotatu ya Bus halijapondeka Sana. Sasa kama
kila mwanafunzi angekuwa kafunga mkanda
wanafunzi waliokaa siti za nyuma wengi
wangepona.
Kwa sababu hakukuwa na seat belt ilipelekea
wanafunzi na walimu wao wote kulushwa mbele ya
gari baada ya gari kukita kwenye kolongo.
2.UZEMBE WA DEREVA
Kuna kila dalili palikuwa na uzembe. Dereva alikuwa
speed kubwa na gari likamshinda kwenye kona
ukizingatia na ubichi wa barabara kutokana na
mvua zinazoendelea.
OMBI LANGU:
wazazi/Waalimu tuwe makini muda wote na hawa
watoto wetu hasa kwenye hizi School Bus, kuna ka
tabia ka kulundika watoto, unakuta seat ya watu
wawili watoto wamewekwa wanne. Inapelekea
watoto kushindwa kufunga mikanda.
Mungu atusaidie!
Jumatatu, 8 Mei 2017
HATIMAYE BAADHI YA MAMBO AMBAYO YALIWEZA KUSABABISHA YAGUNDULIKA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni